Contacts

1sr Floor Shoppers Plaza Tegera Branch, New Bagamoyo Road, Dar es Salaam

+255 776 416 998 or +255 754 500 291

 info@philemonfoundationtz.org

Senior Citizen Club

Fomu ya uanachama ijazwe na kila mwanachama!

MAELEKEZO:

ADA / MICHANGO

1. ADA YA KUJIUNGA
2. ADA YA MWAKA (unaweza pia kulipa kila mwezi)

Tafadhali soma na kuelewa masharti na vigezo vya kujiunga kabla hujajaza Fomu ya Uanachama.

MASHARTI NA VIGEZO VYA KUJIUNGA NA KLABU YA WAZEE YA PHILEMON FOUNDATION

Tafadhali soma kwa makini masharti haya kabla ya kujiunga rasmi na Klabu ya Wazee.

1. Vigezo vya Uanachama

  1. Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 55 au zaidi anaruhusiwa kujiunga.
  2. Kujiunga na Klabu kuwe kwa hiyari na sio kushawishiwa au kulazimishwa
  3. Mwanachana anatakiwa awe tayari kushirikiana na wenzake na awe tayari kushiriki katika shughuli za kijamii na kujitolea.

2. Malipo na Ada
1. Ada ya uanachama na michango mingine ya hiari itapangwa na kuratibiwa na Philemon Foundation.
2.  Malipo yote yatapokelewa kwa njia rasmi kama vile: Selcom, benki, au njia nyingine salama
zitakazotangazwa na Klabu.

3 Ada hazitarejeshwa isipokuwa kwa makubaliano maalum yanayozingatia taratibu za ndani.

3. Matumizi ya Taarifa Binafsi
1. Taarifa zako binafsi zitatumika kwa madhumuni ya ndani ya Klabu tu – kama vile mawasiliano,
mipango ya shughuli, na uchambuzi wa mahitaji ya wanachama.
2.  Hatutauza, kugawa au kutumia taarifa zako kwa faida ya kibiashara.
3. Mfumo huu unazingatia usalama wa taarifa binafsi kulingana na viwango vya faragha.

4. Maadili ya Wanachama
1.  Wanachama wote wanapaswa kudumisha heshima, maadili na ushirikiano wenye kujenga.
2. Klabu haina mrengo wa kisiasa wala kidini. Malumbano, matusi au tabia za uchochezi
hazikubaliki.
3. Mwanachama anahimizwa kushiriki kwa moyo wa kujitolea, kusaidiana na kufarijiana.

5. Shughuli za Klabu
1. Klabu inajumuisha shughuli za afya ya akili na mwili, ujasiriamali, majadiliano ya kizazi, kujitolea
kwa jamii na mentorship.
2. Mwanachama anaweza kualikwa kushiriki au kuongoza baadhi ya shughuli hizi, kwa hiari.

6. Kusitisha Uanachama
1. Mwanachama anaweza kujiondoa muda wowote kwa kutoa taarifa kwa maandishi.
2.Klabu inaweza kusitisha uanachama wa mtu yeyote atakayekiuka maadili ya msingi ya Klabu,
baada ya mazungumzo ya kiungwana.

7. Mabadiliko ya Masharti
1. Philemon Foundation ina haki ya kufanya marekebisho ya masharti haya.
2.Wanachama watapewa taarifa mapema kabla ya mabadiliko kuanza kutumika.

Family Reunion Registration
Jina la Kwanza
Jina la Kwanza
Gender/Jinsia
What are you doing/Unafanya Shughuli Gani?
Terms and Conditions/Vigezo na Masharti